Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipre Jr, Mwalimu mzuri wa masomo yote

Kipre Jr Jr Winga wa Azam FC, Kipre Jr

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni miguu ya Kipre jr pekee ndiyo ilizifanya mbinu za Miguel Gamond kufeli kama mitihani ya Madenge. Wakati mboni zetu zikiwa kwenye starehe ya kushuhudia mzizima Derby, nilikuwa 'busy' kushuhudia miujiza ya Kipre Jr.

Huenda wachache ndio watasadiki ubora wa miguu ambayo iliamua kufunga ndoa ya kanisani na mpira wa miguu. Wale wasiosadiki ubora wake. Kwenye mechi ya Azam sc dhidi ya Yanga walikuwa kwenye jela iliyobeba maonyesho ya picha za maumivu.

Kila jaribio lake lilikuwa kama anachoma kisu kwenye jeraha mbichi linalovuja damu. Ilihali ilikuwa furaha machoni mwa mashabiki wa Azam sc.

Itoshe kusema ndiye winga bora kwa sasa kwenye ligi kuu NBC, achana na magoli yake pamoja na assist zake zinazofurahisha macho ya wengi. Nguvu, kasi, akili zimekuwa silaha kubwa isiyozuilika kwenye miguu yake.

Ni mwalimu wa mawinga wote nchini kwa sasa, nguvu, kasi, akili, zimemfanya kuwa kivutio bora zaidi. . Wakati huu akiandaa 'summary' za topic ya namna ya kuukokota mpira, ni vyema mawinga wa ligi yetu kushika karatasi na peni mapema. kwani ni mwalimu nzuri anayefundisha bila ada. Na Ukitaka somo la 'skills' atakufundisha kama nyongeza.

Ni mawinga wachache sana waliobarikiwa vitu hivi vyote kwa pamoja. Mara ya mwisho mboni yangu ilipata bahati ya kuvishuhudia kwa Simon Msuva na Shiza Kichuya kwenye ubora wake. Ni ukumbusho wa viatu vya Simon Msuva kwenye miguu ya Kipre jr.

Ni ile dhahabu tuliyoigomea kuipitisha kwenye moto. Remember the Name Kipre Jr.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live