Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipindi cha pili kubeba hatma Simba CAF

Half Pic Data Kipindi cha pili kubeba hatma Simba CAF

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MENO ya mashabiki wa Simba nje, unataka kujua imetokana na nani, Mwanaspoti linakuletea uhondo wote kujua kinachoendelea dhidi ya Kaizer Chiefs.

Nahodha wa Wekundu wa Msimbazi, John Bocco ndiye aliyewapa raha hiyo baada ya kufunga bao dakika ya 24, akipokea pasi nzuri ya Claous Chama aliyempasia karibu na 18.

Baada ya Simba kupata bao hilo, walikosakosa mabao jambo ambalo mashabiki lilizidi kuwapa imani ya kuona huenda wanaweza wakaishi ndoto ya kupindua matokeo.

Hii ni mechi ya marudiano, ya kwanza Simba ilipigwa ugenini mabao 4-0 na Kaizer Chiefs nchini Afrika Kusini.

Ili Simba itinge hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itatakiwa kuifunga Kaizer Chiefs mabao 5-0 chini ya hapo itakuwa ndio mwisho wake wa kushiriki michuano hiyo kwa msimu huu.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza Simba inaongozwa kwa bao 1-0, huku wachezaji wakiwa wamekosakosa mabao mengi,jambo ambalo litawapa wakati mgumu kujihakikishia kubaki kipindi cha pili. Lakini kwa upande wa Kaizer Chiefs haijaonekana kuwa na presha kutokana na kuwa na akiba ya mabao matatu mbele hadi sasa, baada ya kushinda kwao 4-0 na yatari wamefungwa bao 1-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz