Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipimo cha MRI, kiboko ya wachezaji wanaodangnya umri

MRI Machine Kipimo cha MRI, kiboko ya wachezaji wanaodangnya umri

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji kudanganya umri si jambo geni hasa Afrika. Tumeshuhudia miaka mingi, tumeshuhudia juzi na jana na tunashuhudia leo na tutashudia hata kesho. Hili limekuwa tatizo sugu likijengeka kwa muda mrefu na kuota mizizi.

Wako wachezaji ambao ukiziona sura zao na maumbo yao ukiambiwa na umri wao, unaweza kubisha mpaka kupigana. Haviendani, hata mtoto mdogo anaweza kubaini na kubisha.

Lakini bahati mbaya hasa barani Afrika, kwa kiasi kikubwa tunategemea vyeti na hati za kusafiria kupima miaka ya mtu, lakini sasa kuanza kutumika kwa teknolojia ikiwemo Magnetic Resonance Imaging (MRI) kumeanza kuwaaibisha wachezaji wengi wanaodanganya umri wao. Ni Nchi Zipi Zimewahi Kuhusishwa na Sakata Hili kwa Afrika?

Nchi wanachama wa Shirikisho la kandanda la Afrika ya kati (UNIFFAC), na nchi za magharibi ni watuhumiwa wakubwa. Taifa la Chad limekua taifa la hivi karibuni kutoka ukanda huo kubainika kudanganya umri kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zilizoanza Januari 12 nchini Cameroon. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.

Lakini siku chache tu kabla ya Chad, wenyeji Cameroon ililazimika kuwatimua wachezaji wake kabla ya kuanza kwa michuano hiyo baada ya kubainika kudanganya umri. Rais wa shirikisho la soka nchini humo Samuel Eto’o , aliamuru hivyo.

Hilo pia limewakuta DR Congo ambao kati ya wachezaji 40 wachezaji 25 walidanganya miaka. Ni aibu, si tu kwa Chad, DRC na Cameroon, ni aibu kwa Afrika nzima. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.

Huko nyuma nchi za Nigeria, Ghana, Tanzania na Kenya ziliwahi kuumbuka na sakata hili. Pia wachezaji tisa kutoka nchi za Congo-Brazzaville, Ivory Coast na Nigeria, watatu kila nchi waliondolewa kwenye michuano ya Afrika ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 nchini Morocco ya mwaka 2013, baada ya vipimo vya kifundo cha mkono vya MRI kuonyesha kuwa wamevuka kikomo cha umri. Somalia yenyewe iliondolewa kabisa.

Kiungo Nurdin Bakari wa Yanga wakati huo aliwahi kubainika na yeye kudanganya umri na kuigharimu timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania U-17, Serengeti Boys kutupwa nje ya mashindano.

Nigeria iliaibishwa na MRI kwenye michuano ya Kombe la Dunia la wachezaji wa chini ya miaka 17 ya 2013. Tatizo ni kubwa na Kipimo cha Magnetic Resonance Imaging (MRI) kinawaumbua. MRI Hutumikaje Kubaini Hili?

Udanganyifu wa miaka limekua donda sugu hasa kwa nchi za Afrika na Asia, ambapo sasa mbali na cheti cha kuzaliwa na hati ya kusafiria, kumekua na teknolojia kadhaa zinatumika kubaini umri wa mchezaji. Mojawapo kubwa inayokubalika inaitwa MRI.

Hiki ni kipimo kisicho cha upasuaji kinachotumika kuchunguza sehemu mbalimbali za mwili, kikitumia mawimbi ya redio, sumaku na kuunganishwa na kompyuta itakayotengeneza picha ambayo itaonyesha sehemu husika inayochunguzwa.

Ni mashine yenye sehemu kuu mbili, ya kwanza ni kitanda ambacho mgonjwa analala na mtambo wenyewe ambapo mgonjwa huingizwa kuchunguzwa tatizo lake. Inaweza kuchunguza sehemu mbalimbali za mwili kama moyo, figo, ini, mapafu,ubongo, bandama, utumbo, kibofu, kongosho, mishipa na maeneo mengine ya viungo vya mwili. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa kwenye mechi zote. Bashiri hapa.

Kwa mantiki ya miaka, hupima kiganja cha mkono wa kulia na hutoa majibu ya kiwango cha umri ambacho muhusika anaweza kuwa nacho.Si rahisi kuidanganya na haiana madhara kwa sababu MRI hazitumii mionzi na majibu yake yanaaminika kisayansi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live