Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipigo cha Yanga kwa Simba chatua bungeni

Simba Vs Yanga Novemba 5.jpeg Kipigo cha Yanga kwa Simba chatua bungeni

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sakata la rushwa kwenye michezo limezua mzozo bungeni leo Jijini Dodoma na mchezo wa wa Kariakoo Dabi iliyochezwa Jumapili Novemba 5, 2023 katika Uwanja wa Mkapa kuhusishwa kuwa na viashiria hivyo.

Yanga iliichapa Simba mabao 5-1 Simba na mabao yakifungwa na Kennedy Musonda kipindi cha kwanza, Maxi Nzengeli akifunga mawili kipindi cha pili, Aziz KI na msumari wa mwisho ulipigwa dakika ya 87 kupitia kwa Pacome Zouzoua kwa mkwaju wa penalti.

Mbunge wa Makete (CCM) Festo Sanga ameibua hoja hiyo akisema kumekuwa na viashiria vya rushwa michezoni ikiwemo mchezo wa Kariakoo Dabi na ameuliza ni upi mkakati wa serikali katika kupambana na rushwa michezoni

"Kwa kuwa kumekuwa na viashiria vya rushwa michezoni na jana tumeona bodi ya Simba imesimamisha baadhi ya wachezaji wakihusishwa na vitendo hivyo ni upi mkakati wa serikali kupambana na vitendo la rushwa michezoni ili ligi yetu iwe bora” amesema Sanga

Akijibu hilo Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema TFF kwa kushirikiana na Takukuru ilianzisha mradi ambao unaitwa kataa upangaji wa matokeo, linda hadhi ya mpira wa miguu ili kukabiliana na rushwa.

“mwanzoni wa msimu huu TFF kwa kushirikiana na Takukuru ilianzisha mradi ambao unaitwa ‘kataa upangaji wa matokeo, linda hadhi ya mpira wa miguu” amesema nakuongeza Mwinjuma

“Ninafahamu hili sio suala linaloweza kutatuliwa ndani ya siku moja malalamiko ni mengi lakini tunafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kupunguza au kuondoa kabisa viashiria na vitendo vya rushwa kwenye mpira wa miguu. Kuthibitisha hilo Takukuru wameanza kutoa elimu kuhusu hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa vitendo vya rushwa au kupanga matokea,” amesema Mwinjuma.

Naye Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Simbachawene ameongeza kabla ya kukalishwa chini na Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu kuwa pamoja na majibu mazuri ya Naibu waziri ameelezea kati ya Takukuru na muungano na vyombo vingine katika kusimamia sekta mbalimbali ikiwemo hii ya rushwa michezoni.

“Rushwa michezoni haikubaliki na kama mchezo wa juzi wa Yanga na Simba unaviashiria vyoyote vya rushwa niwaombe sana klabu ya Simba waende wakaripoti Ofisi ya Takukuru Temeke kama zile tano zimetokana na rushwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live