Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipigo cha Yanga kimevuruga hesabu zetu msimu mzima - Belouizdad

Yanga Cr Belouizdad WA0002 Kipigo cha Yanga kimevuruga hesabu zetu msimu mzima - Belouizdad

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa CR Belouizdad, Marcos César Dias de Castro maarufu kama Marcos Paquetá (65) amesema kuwa kipigo walichokipokea kutoka kwa Yanga SC kimewavurugia mipango yao yote ya msimu huu.

Paquetá amesema hayo kuelekea katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya Makundi ya CAFCL dhidi ya Medeama SC baada ya kukubali kichapo cha bao 4-0 kutoka kwa Yanga na kuondoshwa kwenye michuano hiyo Jumamosi, Februari 24, 2024.

"Matokeo mabaya tuliyoyapata dhidi ya Young Africans yametuharibia mipango yetu mingi na mikubwa msimu huu. Kwanza yametukosesha nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa Vilabu.

"Hii ni kwa sababu sisi ni moja ya vilabu vilivyokuwa na nafasi nzuri ya kushiriki Msimu ujao kutokana kuwa na alama nzuri katika Rank za CAF hivyo kutokana na kutolewa CAFCL hatuwezi tena kufikia malengo haya.

"Pili lengo letu Msimu huu ilikuwa ni kuhakikisha tunacheza Nusu Fainali ya CAFCL lakini hilo pia haliwezekani kwasasa hivyo tumebakiwa na lengo Moja tu kuhakikisha tunamfunga Medeama ili tuweze kupata Pointi zitazotupandisha mpaka nafasi ya 6 katika Rank za CAF," amesema Kocha Paqueta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: