Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipigo cha West Ham chaondoka na Kocha Wolves

Skysports Bruno Lage Wolves 5917500 Bruno Lage

Mon, 3 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wolves imefikia maamuzi ya kumfuta kazi ya ukocha Bruno Lage miezi 16 tangia kuchukua mikoba ya kukinoa kikosi hicho.

Lage, 46, anatimuliwa masaa tu baada ya kukubali kichapo cha bao 2-0 dhidi ya West Ham United mchezo uliochezwa Jumamosi dimba la London.

Kocha huyo raia wa Ureno, ameshinda mchezo mmoja pekee na kupoteza mechi tisa kati ya mechi 15 za Ligi Kuu England baada ya kuichukua timu hiyo mikononi mwa Nuno Espirito Santo ambaye alienda Spurs.

Kwa msimu huu, amefunga magoli matatu akivuna alama sita kwenye mechi nane za EPL.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live