Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipigo cha UEFA kumpa dili Ancelotti

Ederson Morales X Carlo Kipigo cha UEFA kumpa dili Ancelotti

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinda mlango wa Manchester City, Ederson ametoa kauli ya kuushangaza ulimwengu wa wapenda soka juu ya hatma ya Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti.

Ederson amesema;

" Nimeongea na Casemiro, Vinicius na Militão. kuna uwezekano mkubwa Carlo Ancelotti atakuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil. Tutajaribu kuwatoa Real Madrid ili Ancelotti aje kuwa kocha wa Brazil haraka sana " Ederson huyo alimaliza hiyo kauli huku anacheka

Bado Brazil inasaka Kocha wa Timu ya Taifa baada ya kuondolewa patupu katika Fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022.

Hivyo kuondolewa kwa Ancelotti katika michuano ya Ligi ya Mabingwa bila shaka kutasitisha ajira yake kwa wababe hao wa Ulaya, na hivyo itampa nafasi ya kujiunga na Brazil.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live