Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipigo cha Prisons chazidi kuitesa Simba, Mzee Dalali atajwa kuigawa vipande

Mzee Dalali Simba.jpeg Mzee Dalali na Kaluwa.

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanachama wa Klabu ya Simba Mkoa wa Morogoro kupitia Tawi Kuu la Shujaa, lililopo Mji Mpya katika Manispaa ya Morogoro wanadaiwa kuingia kwenye mgogoro mzito uliopelekea kugawanyika makundi mawili Kundi la Wazee na Kundi la Vijana, hii ni baada ya kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons wiki iliyopita.

Awali Simba kupitia Ofisa habari wake Ahmed Ally ulitanga kuhamia mkoani hapa kucheza michezo yake ya Ligi kuu kufuatia Viwanja vya Mkapa na Uhuru vilivyopo Temeke Jijiji Dar es salaam Kufungwa kupisha ukarabati.

Uongozi wa tawi hilo la Shujaa uliipokea timu yao hiyo ambapo lichezo mchezo mmoja tu mkoani hapa dhidi ya Tanzania Prinson na Simba kupokea kichapo cha bao 2-1.



Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya Tawi la Shujaa, matawi yote mawili yanatumia namba moja ya usajili ya klabu (leseni namba 0142), yakichora matawi yao jina moja la Shujaa kila upande ukidai ndio wenye haki ya kumiliki tawi hilo na kuponda uongozi wa tawi lingine.

Kwenye tawi jipya la Shujaa, lililopo kwenye mjego wa Familia ya Mzee Mlanzi, jirani na Stendi ya daladala Kaloleni Mji Mya ikitazamana na Kituo cha Polisi Kata ya Mji Mpya na Zahanati ya Kata ya Mji Mya, imeshuhudiwa mafundi ujenzi wakiendelea kupaka rangi tawi hilo jipya.

HAWA HAPA VIONGOZI WA TAWI HILO

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Muda wa tawi hilo lenye timu yao linaloundwa na wazee wengi wanaodai ndio waasisi wa tawi la Shujaa ambayo ni marafiki wa Simba, Sudi Mrisho Kiwamba amesema;

"Ni kweli sisi tumejiondoa kwenye tawi lile la Shujaa pale Sokoni. Mimi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Tawi, wameniandikia barua ya kunifukuza, ifahamike muda wao wa uongozi umekwisha na hawataki kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi.

"Pia, pale kwenye jengo la CCM wanadai kodi kubwa kama Tsh 1,800,000 na muda wowote wanafukuzwa,” alisema Mzee Kiwamba ambaye kitaaluma ni Mwanasheria na kuongeza, “Shujaa sio tawi la Simba ni timu kamili ya mpira tuliyoianzisha Mwaka 1967 pale nyumbani kwangu namba yetu ya usajili wa timu hiyo.

"Hao kwenye bango, sisi sio tawi la Simba ni marafiki wa Simba katika Tanzania Simba ina marafiki wanne ambao ni Shujaa ya Morogoro, Kikwajuni Zanzibar, Nguvu Moja, Lindi na Nyamaome ya Mwanza.

"Nyamaome na Nguvu Moja zimeshakufa, wale wa pale Sokoni sio Shujaa ni kikundi cha wanachama wa Simba, hatuwatambui kwenye timu yetu kwa sababu hatimiliki zote za shujaa tunazo sisi na mimi ndio Mdhamini wa Mali za Klabu yetu ya Shujaa," alimalizia kusema Mzee Kiwamba huku akionyesha uthibitisho wa kadi yake ya shujaa na Simba.

Baada ya kutoka hapo mwandishi wetu alitinga mtaa wa pili lilipo tawi la awali la Shujaa ambalo liko ndani ya Ofisi za CCM Kata ya Mji Mpya jirani kabisa na Soko Kuu la Kata ya Mji Mpya na kufanikiwa kuzungumza na Mwenyekiti wa tawi hilo Bw Said Mkwinda ambaye amehojiwa na kufunguka haya;

"Hao wapinzani wetu wazee walioasi Shujaa na kwenda pale kwa Mlanzi kuanzisha tawi lao. Shida ni mambo mawili mosi, uroho wa madaraka wa wale wazee na pili makundi ya uchaguzi mkuu wa Simba bado yanaendelea ingawa viongozi wetu waliagiza tuvunje makundi tungane kuijenga Simba yetu, lakini wao hawajavunja kundi lao la Uchaguzi.

"Kila siku wazee wale wanapiga kelele za kutaka kufanyika uchaguzi kinyume na utaratibu, tulishawatangazia wanachama wote kwamba mwezi wa 5 mwaka huu tutafanya uchahuzi, wanachama wametuelewa baadhi ya hao wazee wanapinga.

"Kwenye uchaguzi mkuu wa Simba, wazee wengi wa tawi letu walikuwa timu Moses Kaluwa (ambaye alishindwa na Mangungu). Nasikia hivi karibuni wamewasiliana na Mzee Dalali aliyekuwa akimsapoti Kaluwa na huenda ndiye anayewapa nguvu ya kujiondoa na kuanzisha tawi lao.

"Hakuna mtu aliyefukuzwa, miaka yote tunapokaribia kwenye uchaguzi tunavunja kamati zote ikiwemo kamati ya uchaguzi. Ni kweli Sud Kiwamba ni mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi tumempa barua ya kumjulisha kwamba tumevunja kamati, hatukumpa barua ya kumfukuza tawini.

"Cheti na namba walioandika pale kwenye tawi lao na sisi tunayo hiyo hiyo, tulivyoshinda uchaguzi walitukabidhi wao wenyewe. Kama walitupa cheti na namba feki ya usajili basi hilo ni kosa la jinai kwa sababu tulishinda uchaguzi ule kihalali walipaswa kutupa nyaraka halali na si feki.

"Sisi kudaiwa kodi sio dhambi, taasisi yoyote kudaiwa ni jambo la kawaida kweli hapa CCM tunadeni lakini sio million moja na laki Nane kama wanavyotangaza wahao wapinzani wetu.

"Hapa kodi kwa mwezi tunalipa laki moja na 70 tunadaiwa kama miezi 2 hivi laki tatu na arobaini[340000]na deni hilo tutalipa wakati wowote kuanza sasa. hao wanatangaza hivyo lengo lao CCM watufukuze waje kukaa wao hapa taarifa hizo tunazo.



"Majuzi Mwenyekiti wetu Mangungu kanipigia simu akinipa maelekezo ya maandalizi ya mchezo wetu wa Singida hapa Morogoro. Katika kuthibitisha hilo hata timu yenyewe ya Singida Fountain Gate ilishafika hapa Morogoro, ghafla Azam TV wamedai muonekano wa picha zao pale Jamhuri sio mzuri hivyo wameomba bodi ya ligi kufungia uwanja hiyo ndio sababu ya timu kuondoka Morogoro," amesema Bw. Mkwinda.

Baada ya kichapo hicho ziku kadhaa mbele taarifa kutoka bodi ya Ligi ilitoka na kudai kakao cha pamoja kati ya Simba, Azam Media na Bodi ya Ligi waliketi na kukubari ombi la mwenye haki ya kurusha matangazo kwa maana Azam aliyeomba bodi la ligi kufungia uwanja wa Jamhuri kufuatia uwanja huo kuwa na changamoto nyingi za urushaji matangazo hayo ya moja kwa moja.

HAWA HAPA WADAU WA SOKA MOROGORO

Baadhi ya wadau wa soka mkoani Morogoro waliohojiwa na Mtandao huu waliiga hoja hiyo ya bodi ya ligi kufungia uwanja wa Jamhuri.

“Kwangu mimi hoja hiyo na Bodi ya Ligi naiona ni dhaifu sana, nahisi kuna jambo ligine wala sio hilo. Kufungia Uwanja wa Jamhuri eti una changamoto za kurusha matangazo ya Azam.

"Tumeangalia vizuri gemu ya Simba na Prisons hakuna changamoto yoyote tulioiona. Sasa kama Uwanja wa Jamhuri ulioezekwa na mabati na wapiga picha wa Azam wanakaa vizuri wakiwa comfortable kupiga picha zao vizuri, hivi uwanja wa Manungu ambao hauna mabati au viwanja kama hivyo mbona tunashuhudia picha nzuri za Azam TV? Naona kama watu wa Morogoro tunaonewa kwenye hili," alisema Joseph Banzi.

Credit: Dustan Shekidele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live