Marquinhos amesema Paris Saint-Germain wamechukizwa baada ya kupoteza hapo jana kwenye michuano ya Coupe de France dhidi ya wapinzani wao Marseille.
PSG ililala kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Stade Velodrome siku ya jana, huku bao la kushangaza la Ruslan Malinovskiy katika kipindi cha pili likiweka kumbukumbu ya ushindi kwa wenyeji wa mchezo huo.
Ulikuwa ni ushindi wa kwanza wa Marseille nyumbani katika Mchezo wa Classique tangu Novemba 2011, wakati sasa wanapewa nafasi kubwa ya kuendelea na kushinda shindano hilo waliloshinda mara ya mwisho mwaka 1989.
Marseille walisonga mbele kwa mkwaju wa penalti wa Alexis Sanchez kipindi cha kwanza, ingawa Sergio Ramos alisawazisha bao hilo kabla ya dakika 45 .
Marquinhos amesema kuwa; “Tulikosa vitu, ni wakati wa kufunga midomo yetu. Tunajua tunapaswa kuimarika zaidi ikiwa tunataka kufanya mambo mazuri msimu huu. Taji ambalo linaondoka, linaumiza. Tumechukizwa.”
Beki huyo wa kati ameongezea kuwa walijua wangefanya kazi nyingi, lakini hawakuweza kupita njia zao kwa kasi zaidi. Walifanya makosa machache ambayo yaliwagharimu sana. Wanajua wanachohitaji kuboresha na ni kichapo ambacho kinaumiza kwasababu ni mechi ya Kombe dhidi ya mpinzani wao mkubwa.
Wakati huo huo kocha mkuu wa PSG Christophe Galtier amekiri kuwa upande wake ulikuwa unapambana kukabiliana na kupoteza mchezo huo. Inasikitisha sana. Coupe de France ilikuwa moja ya malengo yao na walifungwa na timu kubwa ya Marseille na ilikuwa ngumu kutengeneza nafasi. Alisema kocha huyo.
“Wachezaji wamekata tamaa, wamezidiwa. Sio wakati wa kuongea kwa hasira, inabidi tuendelee na kazi, tujikite.”
Ingawa PSG itazingatia kurejea Ligue 1 kabla ya kuelekeza mawazo yao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa na Bayern, Marseille wanaweza kutazamia kufuzu kwa robo fainali.
Alipoulizwa kama kukosekana kwa Kylian Mbappe kutokana na jeraha kuliwapa Marseille ujasiri wa kusonga mbele zaidi uwanjani, Guendouzi alijibu: “Hapana, kama tulivyoona, katika mchezo wa kwanza dhidi ya PSG, kipigo cha 1-0 cha Ligue 1 mnamo Oktoba tulishambulia sana.”
“Tunajiamini, tunajiamini kwa mabeki wetu. Bado kuna mechi nyingi kabla ya kwenda kushinda Coupe de France. Ni timu ambayo itaenda kwa moyo.”