Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipigo cha 5-1, kejeli bado zinaendelea Simba

Yanga Bango Kipigo cha 5-1, kejeli bado zinaendelea Simba

Sat, 18 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba ikiendelea kukerwa na mabango ya matokeo ambayo watani wao Yanga wameyatengeneza, Bodi ya Ligi ya Tanzania nao wameitengeneza lao kimtindo.

Kupitia ripoti ya Kamati ya Usimamizi iliyotolewa jioni ya jana imezipiga faini Simba na Yanga kupitia matukio mawili tofauti yaliyojiri kwenye mechi hiyo namba 45 iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Novemba 5, 2023.

Yanga wao wamekumbana na faini ya sh5 milioni kwa kosa la timu yao kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.

Simba wao adhabu Yao ikawa ya sh1 milioni kwa kosa la kuchelewa kuingia uwanjani na kuharibu ratiba ya kuanza kwa mchezo huo kwa dakika nne.

Faini hizo mbili zimezusha kejeli mitandaoni zikionyesha kamati hiyo imekumbushia matokeo ya mchezo huo kwa Yanga kushinda kwa mabao 5-1 kupitia adhabu hizo kwa klabu zote mbili.

Yanga baada ya ushindi huo wamekuwa na muendelezo wa kuwatania watani wao kwa kubandika mabango mbalimbali ya kulipia sehemu mbalimbali za Jiji yakikumbushia matokeo hayo.

Mabango hayo yamekuwa yakiwakera mashabiki wa Simba huku wengine wakiishauri  klabu hiyo kufungua kesi mahakamani kudai fidia kwa klabu yao kupitia mabango hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live