Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa wa Stars alietunguliwa na Morocco atoa neno

Kawawa Stars Kipa wa Stars alietunguliwa na Morocco atoa neno

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wageni wao Morocco ‘mechi’ ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 iliyopigwa jana Uwanja wa Mkapa, ‘golikipa’ Kawawa atoa neno baada ya ‘mechi’ hiyo.

Mlinda mlango huyo aitwaye Kwesi Kawawa ametoa shukurani kwa kuchaguliwa kucheza katika mchezo huo kwani ni mechi yake ya kwanza ya kimataifa kufuzu kombe la dunia hivyo basi ni matuamaini yake watarudi wakiwa imara.

Kwasi ameeleza kuwa amefurahishwa sana na ‘sapoti’ ya watanzania na amepokea maoni yao na atayafanyia kazi.

Kwasi alikuwa mlinda mlango katika mechi iliyochezwa usiku wa kuamkia leo ambapo mabao ya Morocco yalifungwa na HakimZiyech na Lusajo Mwaikenda akijifunga bao la pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live