Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa namba moja wa Cameroun atimuliwa kambini

Andre Onana Ksl Andre Onana

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa namba moja wa timu ya Taifa ya Cameroon, Andre Onana (26) ambae anaichezea klabu ya Inter Milan ametimuliwa kambini na benchi la Ufundi la Cameroon kwa sababu za kinidhamu.

Inasemekana kuwa kipa huyo amekuwa na matukio ya utovu wa nidhamu ndani ya kambi ya timu hiyo.

Onana alicheza mechi ya kwanza dhidi ya Switzerland ambapo Cameroon iliambulia kichapo cha bao 1-0 na sasa nafasi yake imechukuliwa na Devis Epassy.

Zipo taarifa zinazodai kuwa Onana ambaye ana michezo 34 kwa Cameroun ameachwa na kocha wake Rigobert Song baada ya kumwambia abadilishe staili yake ya kucheza kwani anacheza kizamani jambo ambalo lilimkera kipa huyo na kumfokea kocha wake.

Aidha, zipo taarifa nyingine zinazodai kuwa mchezaji huyo alikikataa kikosi cha Timu hiyo alichopanga kocha dhidi ya Serbia huku nyingine zikidai kuwa amehoji kwa nini Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroun, Samuel Etoo amekuwa akiingilia maamuzi ya benchi la ufundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live