Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa mpya aipaisha Yanga Afrika

Diarra Pic Data Kipa mpya aipaisha Yanga Afrika

Fri, 27 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Siku chache baada ya kusajiliwa na Yanga, kipa Djigui Diarra ameanza kuipa chati timu hiyo baada ya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Mali kinachojiandaa na mechi mbili za kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ha Rwanda na Uganda mapema mwezi ujao.

Kuitwa kwa Diarra ni muendelezo wa kipa huyo kuwemo katika kikosi cha Mali ambacho amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu.

Ni kikosi cha wachezaji 28 ambacho Kocha wa Mali, Mohamed Magassouba  amekitangaza, kikiwa na mchezaji mmoja tu anayecheza ligi ya nyumbani huku 27 waliobakia wakiwa wanacheza soka la kulipwa katika klabu mbalimbali barani Ulaya na hapa Afrika.

Idadi kubwa ya nyota walioitwa ni wale wanaocheza katika klabu mbalimbali huko Ufaransa lakini pia kuna waliopo katika klabu za England, Italia na Ujerumani mtawalia.

Wachezaji hao 28 wanaounda kikosi cha Mali kilichotangazwa leo ni Diarra (Yanga), Ibrahim Mounkoro (TP Mazembe), Mohamed Niare (Stade Malien), Ismael Diawara (Malmo), Hamari Traore (Rennes), Falaye Sacko (Guimares), Charles Traore (Nantes), Mamadou Fofana (Amiens), Boubacar Kouyate (Metz), Senou Coulibaly (Dijon) na Mahame Siby (Strasbourg)

Wengine ni  Diadie Samassekou (Hoffenheim), Lassana Coulibaly (Salernitana), Aliou Dieng (Al Ahly), Mohamed Camara (Red Bull Salzburg), Cheick Dacoure (Lens), Amadou Haidara (Leipzig), Kouame Rominigue(Troyes), na Mouss Djenepo (Southampton)

Pia kuna Adama Traore (Sheriff Tiraspol), Moussa Doumbia (Reims), Ibrahim Kane (Vorskla), El Bilal Toure (Reims), Ibrahim Kone (Sarpsborg), Mahamadou Doucoure (Nimes), Lassine Sinayoko (Auxerre) na Hamidou Sinayoko (Createurs)

Septemba Mosi, Mali itaikaribisha Rwanda na baada ya hapo itasafiri hadi Kampala kuikabili Uganda, Septemba 6

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz