Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa la penalti DRC latoa neno

Mpila Kipa la penalti DRC latoa neno

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa DR Congo,anaamini nchi yake itatwaa ubingwa wa Afcon nchini Ivory Coast kama ilivyotwaa ubingwa wa CHAN 2009 nchini humo.

Mpasi alifunga penalti ya ushindi na kuiwezesha DR Congo kuing’oa Misri katika hatua ya 16-Bora.

Kipa huyo anafananisha mwendo wa DRC katika Afcon 2023 na mafanikio yao kwenye CHAN iliyofanyika Ivory Coast pia miaka 15 iliyopita.

“Tunaenda kupumzika vyema kisha tutaanza kupiga hesabu za mechi baada ya mechi. Hii ni bila ya kusahau kwamba DR Congo ilitwaa ubingwa wa Afrika hapa Ivory Coast (CHAN 2009). Pengine hii ni ishara,” alisema.

Kipa huyo alifafanua namna alivyohakikisha penalti ya kipa wa Misri, Gabaski haiingii golini mwake na mbinu aliyotumia kufunga penalti yake.

“Nilijaribu kuwa mtulivu. Niljaribu kumvuruga Gabaski asipige vizuri na nikafanikiwa. Baada ya hapo, nikatuliza akili na kutumia ufundi kiusahihi,” alisema kipa huyo wa Congo DR.

Mpasi alisema anakumbuka alivyokosa penalti mazoezini na akajaribu kupiga vizuri zaidi.

“Kabla sijapiga penalti yangu, nilikumbuka namna nilivyokosa mazoezini, lakini hapa ikaenda vyema,” alisema.

Beki wa Simba, Henock Inonga pia alifunga penalti wakati DRC ikiilaza Misri kwa penalti 8-7 baada ya mechi yao kumalizika kwa sare ya 1-1.

DRC ambayo robo fainali itacheza dhidi ya Guinea Ijumaa hii, imeshinda ubingwa wa Afcon mara mbili, 1968 na 1974, na tangu hapo mafanikio ya juu zaidi ni kumaliza washindi wa tatu mwaka 1998 na 2015.

Chanzo: Mwanaspoti