Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa huyu atajwa kumrithi Manula Simba

Ndikumana Justin Kipa huyu atajwa kumrithi Manula Simba

Sat, 13 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya simba kwa sasa imeingia sokoni kutafuta nafasi ya Aish Manula kwa kujikuta wako katika hekaheka moja na klabu ya Singida SBS na Geita Gold katika kuwania Saini ya Golikipa wa Coastal Union.

Justine Ndikumana (30) raia wa Burundi aliyetokea nchini Kenya kuja kutumikia Timu ya Tanzania anamkataba wa miaka miwili na klabu ya Coastal Union kwa sasa.

Chanzo changu cha habari kinaeleza kuwa Moja wapo ya viongozi waliongea nasi "Ndikumana ni kipa mzuri ambaye amecheza kwa muda mdogo na kuonesha kiwango kikubwa akiwa na Coastal Union" - (Hakupenda Atwaje jina).

Tangu ajiunge na Coastal Union amecheza michezo 7 ambapo katika michezo hio amefungwa magoli matatu tu tangu acheze klabuni hapo, na mpaka sasa anamiaka 09 tangu aondoke nchini Burundi kutumikia vilabu vya nje ya nchi yake.

Tulipomtafuta Kipa uyo alisema kuwa anaheshimu mkataba wake na Coastal Union kwa sasa hawezi sema kuwa akihitajika ataenda au lah!!!

Tulipozungumza na semaji la Coastal Union alieleza kuwa kila kitu kinawezekana lakini utaratibu muhimu, uongozi ufatwe taratibu zifatwe pia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live