Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa baada ya kufungwa asema Haaland 'Sio binadamu'

Haaland Grealish .jpeg Kipa baada ya kufungwa asema Haaland 'Sio binadamu'

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Erling Haaland, 22, baada ya kuwa na mwanzo mzuri kwenye kikosi cha Manchester City kumemfanya golikipa wa FC Copenhagen, Kamil Grabara kushindwa kujizuia na hivyo kujiuliza maswali kuwa Mshambuliaji huyo ni binadamu kweli.

Kiungo mshambuliaji wa Man City, Jack Grealish alisema baada ya Haaland kufunga, kipa Grabara alimfuata na kumwambia ‘Haaland sio binadamu’ jambo ambalo lilimfanya jack abaki akishangaa kutokana na kauli hiyo ya kipa wa wapinzani wao.

Haaland aliyefunga magoli mawili kati ya matano waliyopata City, yanamfanya kufikkisha jumla ya mabao 19 kwenye michezo 12 aliyocheza tangu kujiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya Borussia Dortmund.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 hata hivyo hakumaliza dakika zote 90, na badala yake alipumzishwa na kocha Pep Guardiola pengine alikuwa na nafasi ya kufunga ‘hat-trick’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live