Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Singida: Nilidaka mpira ukiwa nje

Singida F91a642 Kipa Singida: Nilidaka mpira ukiwa nje

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kelele zikiendelea kuwa nyingi juu ya shambulizi la kona katika mchezo wa Singida Fountain Gate dhidi ya Simba wadau watofautiana.

Kipa wa Singida Fountain Gate Ibrahim Parapanda amesema mwamuzi Nasri Salum 'Msomali' hakufanya maamuzi ya haki kwa kuwapa shambulizi la kona Simba kwa kuwa wakati anaudaka mpira tayari ulishakuwa umetoka.

Parapanda amesema wakati Msomali anaamua kuwa kona tayari mwamuzi wa kwanza msaidizi alitofautiana naye akisema mpira umetoka na upigwe kuelekea Simba.

"Namshangaa sana Msomali kwa kile alichoamua, kwanza ujue Mimi alishanionya kwamba nisipoteze muda, kwahiyo ule mpira wakati Saido (Said Ntibazonkiza) anaupiga haukumgusa mchezaji wetu yoyote na mimi nimeudakia nje ili nisipoteze muda tupige haraka kwa kuwa alishawaongezea sana muda,"amesema kipa huyo.

"Nikamwambia amuangalie hata msaidizi wake ameweka tupige sisi akawa hataki kutusikiliza akasimamia maamuzi yake, yule beki wa Simba Hussein Kazi alijua kwamba ule mpira ukitoka hautakuwa kona ndio maana alikuwa anataka kuuwahi usitoke haya yote hakutaka kuyaona kama yangemsaidia basi hata angekwenda kwa msaidizi wake amsikilize hakutaka,”

Naye kocha msaidizi wa Singida Nizar Khalfan amesema hata kama muda ulipotezwa lakini haukuwa kwa kiwango ambacho Msomali aliongeza huku pia akiwatupia lawama wapangaji wa waamuzi hao kwa hatua ya kumpanga mwamuzi huyo kwenye mechi zao zote mbili

"Sisi kwenye mashindano haya tumekutana na Simba mara mbili na mara zote kapewa mwamuzi huyu huyu tuanze kujiuliza Yuko peke yake? Angalia ile kona aliyowapa, hata kama muda ulipotezwa sio kwa kiwango ambacho aliongeza ikionyesha wazi kwamba alikuwa na hesabu zake.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Waziri Shekha amesema baada ya kikao kilichofanyika leo Januari 11, 2024 kupitia ufanisi uliofanywa na Msomali na wasaidizi wake wamegundua kwamba mwamuzi huyo hakuwa sahihi kwenye uamuzi wake huo wa kuwapa kona Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live