Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Singida Big Stars "Mlitaka nifanyeje?"

Singidani Smb Kipa Singida Big Stars "Mlitaka nifanyeje?"

Sat, 12 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Singida Big Stars, Abubakar Khomen amesema bao alilofungwa kwenye mechi dhidi ya Simba hata mfungaji, Peter Banda hakutegemea kama angeweza kuupiga ule mpira vile.

Khomen alisema dhumuni la Banda ilikuwa ni kupiga krosi bahati mbaya alikosea na kupiga mpira uliokwenda langoni.

Alisema wakati anasogea mbele ya goli ili kuibia krosi ya Banda kwa bahati mbaya mpira ulibadili uelekeo akiwa kwenye harakati za kuokoa ukaingia wavuni.

“ Mara zote makipa huwa tunafundishwa kabla ya krosi kupigwa natakiwa kuibia na hilo ndio ambalo nilifanya bahati mbaya mpira ulikwenda tofauti na vile ambavyo nilikuwa natarajia,” alisema Khomen na kuongeza;

“Kosa la kimpira ambalo limetokea na nitakwenda kulifanyia kazi zaidi kwenye uwanja wa mazoezi ili kubadilika kabla ya kucheza michezo ijayo.”

Bao la Singida kwenye mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1, Uwanja Liti Singida lilifungwa na Deus Kaseke baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa kiungo Said Ndemla.

Wakati huohuo, Ndemla alisema kucheza dhidi ya Simba haikuwa kazi rahisi kwani ni miongoni mwa timu kubwa nchini yenye wachezaji wazuri katika kila eneo.

Ndemla alisema alitenga muda wa kutosha kufanya mazoezi ya timu kwa pamoja muda wa ziada kufanya mazoezi binafsi=.

“Ilikuwa lazima nipambane vya kutosha kwani wachezaji wengi wa Simba tunafahamiana lisingekuwa jambo bora kwangu kucheza kwenye kiwango cha chini dhidi yao,” alisema Ndemla aliyekuwa kuwa na Simba kwa muda mrefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live