Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Simba SC afiwa na mama yake

Kakolanya Beno.png Golikipa wa Simba SC, Beno Kakolanya

Thu, 19 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kipa wa Simba, Beno Kakolanya leo Agosti 19, 2021 asubuhi  amefiwa na mama yake mzazi anayeitwa Eva Mwankusye na msiba upo kwao Isyesye jijini Mbeya.

Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na kaka wa mchezaji huyo, Asajile Mwakalindile ambaye alikuwa na mama huyo muda wote.

Mwakalindile amesema; ”Ni kweli mama amefariki leo asubuhi na bado tupo hospitali, tutaendelea kuwapa taarifa kwa kadri tutakavyopanga”

Mke wa Kakolanya anayefahamika kwa jina la Hadra, aliliambis Mwanaspoti mama mkwe wake ni kweli amefariki na anamsubiri mumewe arejee ili waweze kusafiri kwenda Mbeya.

Kakolanya yupo nchini Moroccco  na kikosi cha Simba katika maandalizi ya msimu mpya lakini anatarajia kurejea nchini kesho kwa ajili ya mazishi ya mama yake.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz