Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Serbia apigana na shabiki

Kipa Pict.png Kipa Serbia apigana na shabiki

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa timu ya taifa ya Serbia, Vanja Milinkovic-Savic anadaiwa kuwa alipigana na shabiki baa siku moja kabla ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kati ya taifa lake na Denmark.

Taarifa kutoka gazeti la Serbia Telegraf zinadai  Milinkovic-Savic alikwenda kwenye baa moja jijini Munich siku ya mapumziko kabla ya mechi dhidi ya Denmark. Inadaiwa shabiki mmoja alimuona mchezaji huyo na kumhoji kwanini hakuwa kambini na wenzake kujiandaa na mechi ya mwisho ya makundi.

Baada ya mchezaji huyo kuulizwa hasira zilimpanda kipa huyo anayedaiwa kwamba alimsukuma shabiki huyo kisha akampiga ngumi. Baada ya hali hiyo, walinzi wa baa waliingilia kati na kuwatenganisha wawili hao.

Jarida moja la Serbia lilifanya mahojiano na mmiliki wa baa hiyo ambaye alisema tukio hilo halikumhusisha kipa huyo na shabiki, bali ilikuwa ni dhidi ya walinzi.

“Vanja alikuja kwenye baa yetu, lakini walinzi wa mlangoni hawakumtambua na hawakutaka kumruhusu aingie ndani kwa sababu alikuwa amevaa bukta ya timu ya taifa, jambo ambalo lilimkasirisha na kusababisha vurugu zianze,” alisema meneja huyo.

“Haraka haraka niliingilia kati nikamshika mkono na kumwambia aingie na mimi, lakini alikataa. Lakini mwisho tulisuluhisha ugomvi na kila kitu kikaenda kama kilivyopangwa.”

Milinkovic-Savic ambaye anaichezea Torino ya Italia hakubahatika kucheza mechi yoyote katika michuano hiyo licha ya kuwa sehemu ya kikosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live