Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Nigeria: Ivory Coast tutauana

Kipa Nigeria Kipa wa Super Eagles, Stanley Nwabali

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Super Eagles, Stanley Nwabali amesema tena kwa msisitizo hakuna namna nyingine ya kuisaidia Nigeria kusonga mbele kwenye fainali za Afcon 2023 zaidi ya kuwafunga wenyeji wa mikikimikiki hiyo, Ivory Coast katika mchezo wao ujao.

Mastaa wa Nigeria wanapasua kichwa juu ya kiwango chao cha sasa na mpinzani wanayekwenda kukutana naye baada ya kushinda mechi moja kati ya nne za mwisho, huku mechi yao ya kwanza kwenye Afcon 2023 ilibanwa na Equatorial Guinea na kutoka nao sare ya bao 1-1.

Kipa, Nwabali ambaye aliidakia Super Eagles kwa mara ya kwanza alisema juu ya umuhimu wa kuwashinda Ivory Coast na kusema mchezo wa kwanza haukuwa mzuri kwake.

“Ile mechi ya Equatorial Guinea haikuwa nzuri kabisa kwangu. Lakini, najua kipi kinachopaswa kufanya,” alisema.

Ivory Coast maarufu kama Tembo ndio wanaoongoza Kundi A baada ya kukusanya pointi tatu kutokana na ushindi wao wa mabao 2-0 kwenye mechi ya kwanza ya fainali za Afcon 2023 dhidi ya Guinea-Bissau.

Kipa Nwabali alisema ugumu wa mchezo wa Ivory Coast, lakini ushindi ndiyo utakaowaweka kwenye hali nzuri ya kusonga mbele, akisema:

“Hii ni mechi ya lazima ushindi. Nafahamu mechi ni ngumu, lakini ni lazima tushinde.” Mechi ya Super Eagles na Ivory Coast itapigwa kesho, Alhamisi.

Chanzo: Mwanaspoti