Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Dodoma Jiji afichua siri yake na Medo

Mohamed Mohamed Kipa Dodoma Jiji afichua siri yake na Medo

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Dodoma Jiji,Melis Medo mpaka sasa ameshafundisha timu tatu Ligi Kuu tangu ametua hapa nchini, lakini kipa Mohamed Husein Mohamed ambaye amekuwa akiambatana na mmarekani huyo amesema siri kubwa inayomfanya aive naye ni nidhamu na kujituma kwake.

Medo alimkuta kipa huyo kinda kwenye kikosi cha Gwambina ambapo alimwamini na kuanza kumpanga kisha badaye akatimkia Coastal Union ambapo alimvuta Mohamed na kumpa nafasi ya kuanza kwenye timu hiyo na sasa kocha huyo yupo Dodoma Jiji na yupo naye kwenye klabu hiyo.

Kipa huyo amesema ukitaka kuelewena na kocha huyo basi lazima kwanza ujitume kuanzia mazoezini hadi kwenye mechi atakayokupanga na pia uwe na nidhamu kubwa kitu ambacho yeye alishamsoma mmarekani huyo na ndio sababu kubwa ya kuwa naye kwenye timu tatu alizofundisha mpaka sasa.

Mohamed amesema anamshukuru sana kocha huyo kwani ndiyo aliyempa nafasi ya kuonyesha kipaji chake wakati yupo Gwambina na kumfanya apate uzoefu mkubwa wa kucheza mechi za Ligi Kuu na sasa amekomaa.

“Unajua Medo ni kocha mzuri sana ila ukitaka uwe naye karibu basi uwe na nidhamu na kujituma yeye anapenda muda wa mazoezi ufike kwa wakati, uwe msikivu na ujitume kwenye mechi na mazoezini ukifata hivyo basi mtakuwa pamoja.

“Mimi hilo ninalifanya ndio maana unaona mpaka sasa niko naye alianza na mimi kule Gwambina na kisha akanichukua Coastal Union na sasa nipo naye Dodoma Jiji kwangu ni kama mzazi wangu hivyo namshukuru sana kwani amenikuza na sasa nimekuwa mzoefu wa Ligi Kuu,” alisema Mohamed.

Chanzo: Mwanaspoti