Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Azam afichua kinachombakiza Bara

Mohamed Mustafa Azam Mohamed Mustapha

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Azam FC, Mohamed Mustafa amesema licha ya kuichezea Ligi Kuu Bara kwa miezi sita tu akiwa na kikosi hicho ila amevutiwa na jinsi mashabiki wanavyozipenda na kuzifuatilia timu wanazozipenda tofauti na mataifa mengine Afrika na ndio kubwa lililomfanya aamue kusalia na kikosi hicho kilichomtoa Al Merrikh.

Mustafa alijiunga na Azam katika dirisha dogo la msimu uliopita akitokea Al-Merrikh ya Sudan na amekuwa nguzo imara ya mafanikio ya Wanalambalamba iliyoakata tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupita miaka 20 na kuwafanya mabosi wa Azam kuanza mazungumzo ili kumsajili moja kwa moja.

Akizungumza na Mwanaspoti Mustafa alisema, soka la Tanzania limeonyesha ni bora katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati na hajashangazwa kuona wachezaji wakubwa na wenye wasifu mkubwa kutoka mataifa mengine wakivutiwa kuchezea nchini.

“Ligi ya Tanzania ni bora na nimevutiwa na vitu vingi, ingawa jambo kubwa nimependa jinsi mashabiki wanavyozipenda timu wanazoshabikia, kumekuwa na mijadala ya mara kwa mara kitu ambacho kinaifanya kupiga hatua nje ya mipaka,” alisema Mustafa aliyemaliza ligi akiwa na clean sheet nane.

Aidha Mustafa aliongeza, shauku yake kubwa ni kuendelea kucheza hapa nchini ingawa suala lake amewaachia viongozi kwani wao ndio watakaolishughulikia, huku akiweka wazi amependezwa na mazingira ya Tanzania na ushindani uliopo katika Ligi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ akizungumzia kuhusu usajili wa nyota huyo moja kwa moja ndani ya kikosi hicho alisema, bado hawajakamilisha hilo na litakapokamilika wataweka wazi katika mitandao yao ya kijamii.

Mustafa amekuwa muhimili mkubwa ndani ya timu hiyo ambapo amekuwa panga pangua kikosi cha kwanza ambacho amekiwezesha kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara na kukata tiketi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Chanzo: Mwanaspoti