Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kipa Afrika Kusini alivyoipeleka Nigeria fainali

Stanley Nwabili Stanley Nwabili.

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ilikuwa ni zamu ya kipa wa Chipa United ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Stanley Nwabili akionyesha ufundi wake wa kupangua penalti mbili za Afrika Kusini akiibeba Nigeria kutinga Fainali ya michuano ya Afcon 2023 inayoendelea Ivory Coast.

Furaha ilizidi kwa Nigeria baada ya penalti ya mwisho ya Kelechi Iheanacho kwa mabingwa hao mara tatu wa kombe la Afcon ikiifunga  Afrika Kusini kwa mikwaju minne kwa miwili kwenye mchezo wa nusu fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Bouake, Ivory Coast.

Niageria ambayo ilikuwa ya kwanza kupiga penalti, ilifunga penalti hizo nne za Terem Moffi, Kenneth Omeruo, William Troost-Ekong na Iheanacho, huku Ola Oina akikosa moja kwa Nigeria.

Kwa upande wa Afrika Kusini ilipata mbili za Mihlali Mayambela na Mathobi Mvala huku Tobeho Mokoena na Evidence Makgopa wakikosa.

Nigeria ilianza kupata bao la kwanza la nyota wa klabu ya PAOK inayoshiriki Ligi Kuu ya Ugiriki, William Troost-Ekong  kwa mkwaju wa  penalti dakika ya 67 baada ya Victor Osimhen kuangushwa eneo la hatari na Mothobi Mvala, huku Afrika Kusini ikisawazisha dakika ya 85, kwa penalti ya Mokoena  baada ya Percy Tau kuangushwa na alhassan Mohamed eneo la penalti n mchezo huo kumalizila kwa sare ya bao 1-1 hadi dakika 120 zikimalizika baada ya kuongezwa 30 na kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Nigeria ambayo  ilitawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa, ilikuwa na kosa kosa nyingi ikiongozwa na mshambuliaji wa Napoli ya Italia, Osimhen na kumpa wakati mgumu kipa wa Afrika Kusini, Ronwen Williams aliyeibuka shujaa Bafana Bafana ikifuzu nusu fainali dhidi ya Cape Verde akipangua penalti nne kwenye kupigiana penalti tano kila moja.

Nigeria imebeba mataji matatu ya Afcon, mwaka 1980 fainali zilizofanyika nchini kwao, 1994 ilibeba fainali za Tunisia na 2013 zilizoandaliwa Afrika Kusini, huku Afrika Kusini ikibeba mara moja kwenye fainali zilizofanyika nchini kwao mwaka 1996.

Kabla ya mchezo huu, Afrika Kusini ilikuwa haijapoteza kwenye mechi nne mfululizo za fainali za Afcon ikishinda mbili na kutoa sare mbili, ikiwa ni nyingi kuliko ilivyocheza michezo 21 kabla.

Afrika Kusini hii ni nusu fainali ya nne kwenye Afcon na ya kwanza tangu mwaka 2000 ilipopoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Nigeria.

Nigeria na Afrika kusini zimeshinda mechi zao nne za mwisho na mara ya mwisho kukutana kwenye nusu fainali ni mwaka 2000 na Super Eagle ilishinda mabao 2-0 ya Tijan Babangida.

Nigeria itakutana na mshindi wa mchezo wa Ivory Coast dhidi ya DR Congo, huku Afrika Kusini ikisubiri matokeo ya mchezo huo kucheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live