Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kioja! Giroud achaguliwa Golikipa Bora wa wiki Serie A

Giroud Goliekeeper Kioja! Giroud achaguliwa Golikipa Bora wa wiki Serie A

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Olivier Giroud ambaye anachezea AC Milan ya Italia amechaguliwa kuwa golikipa bora wa wiki wa Ligi Kuu ya a Italia ya Serie A baada ya michezo ya raundi ya 8 ya Ligi hiyo.

Itakumbukwa Giroud alilazimika kuvaa glavu (gloves) na kukaa langoni baada ya golikipa wa klabu hiyo, Mike Maignan kuoneshwa kadi nyekundu. Giroud aliokoa michomo kadhaa na kuisaidia AC Milan kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Genoa siku ya Jumamosi.

Kufuatia hilo, AC Milan tayari imeanza kuchapisha na kuuza jezi ya golikipa wa klabu hiyo yenye jina la Giroud mgongoni hivyo mashabiki wa Soka wataweza kununua jezi ya klabu hiyo ikiwa na jina la Olivier Giroud mgongoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live