Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinyago cha Victor Osimhen kinamvyotisha Rashidi Yekini

Victor Osimhen.jpeg Victor Osimhen

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati dunia ikiangaika na kuzalisha wachezaji kutoka kwenye maabara ya soka.

Ni bara la Afrika pekee limegoma kuingia maabara, Ardhi ambayo hata 'kopi' zake ni adimu kupatikana duniani bali ni vipaji halisi.

Afrika iliwahi kutuletea Yaya toure, Rashid Yekini, Jay Jay Okocha, ni baadhi tu ya mbegu ambazo maabara nyingi zilijaribu kuiba 'kopi' zake lakini walishindwa.

Hauwezi kumtengeneza Victor maabara, ni muendelezo wa mbegu adimu ambazo waafrika tumeamua kuzifunika kwenye udongo uliobarikiwa. Ni zile mbegu ambazo ziliachwa na Didier Drogba na Samuel Eto'o, Rashidi Yekini, na Jay Jay Okocha.

Baada ya miaka mingi kupita ya utawala wa Rashidi Yekini, wanaigeria wametuletea mbegu nyingine kutoka mitaa ya Ojota, Victor Osimhen.

Wanaigeria jina lake hawakuwa wanaliimba kwa bahati mbaya, ulikuwa ni muendelezo tu wa kulitukuza jina lake, kabla yao mioyo ya Napoli ilikuwa tayari imeshapigwa chapa ya moto jina la Victor Osimhen kwenye mioyo yao.

Kama ilivyo ngumu kumuona Mange kimambi akiacha umbea, na ni hivyo ilivyo ngumu kumuona Victor Osimhen akiacha kuzitendea ukatili nyavu.

Yupo nafasi ya nne hadi sasa kwenye ile orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa wanaigeria akiwa na mabao 20.

Kwenye orodha ya kuzitendea hila nyavu. Kiongozi wao ni Rashidi Yekini na mabao yake 37. ni mabao 17 punguzu kwa Victor Osmhen

Kinyango cha Victor Osmhen kimeanza kumtisha Rashidi Yekini. Ni kana kwamba ni suala la muda tu kabla Victor kuwa kileleni kwenye orodha ile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live