Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kingereza chamfukuzisha kazi Kocha Leeds United

 126857158  Am50287 Kocha Brian McDermott

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmiliki wa zamani wa Klabu ya Leeds Utd Massimo Cellino hivi karibuni ameeleza jinsi ugumu wa matumizi ya Lugha ya Kiingereza baina yake na Kocha Brian McDermott ulivyopelekea yeye kuchukua uamuzi wa kumtimua ndani ya Klabu hiyo :

“Nilipofika Leeds United kwa mara ya kwanza nilikuwa na moto, halafu Kiingereza changu kilikuwa kibovu sana hata matamshi yangu tu yalikuwa ya shida sana."

"Sasa wakati naingia kwa mara ya kwanza ndani ya makao makuu ya Klabu, lilikuwepo kochi la rangi ya zambarau kwenye ofisi yangu lakini lile kochi sikulipenda hivyo nikaomba libadilishwe."

"Nikamwambia CEO wa Timu ‘Badilisha hilo kochi sijalipenda ni baya, sitaki kuliona tena.’ kumbe nilikosea badala ya kusema KOCHI nikasema KOCHA."

"Nikawa nimekaa ofisini mpaka jioni, CEO akanifuata akaniuliza ‘Nani ataiongoza timu kwenye mchezo wa kesho?’ nikamuuliza kwa mshangao, ‘Kwani kuna nini?' Kocha si yupo?’. Wakaniambia, ‘Ulisema asubuhi tumfukuze na ndicho kilichofanyika.’

"Nakumbuka ilikuwa mida ya saa 10 jioni na kulikuwa na mashabiki zaidi ya 2,000 kwenye Uwanja wetu.Mashabiki kidogo wanitoe roho kisa nimemfukuza Kocha bila sababu za msingi."

"Lakini nashukuru Polisi walinificha kisha wakanitoa ofisini kwa kutumia Gari lao." Massimo Cellino, Mmiliki wa zamani wa klabu ya Leeds United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live