Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinda Mtanzania kupeperusha bendera Russia

Harrith Chunga Misonge Pic Harrith Chunga Misonge.

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kinda wa Tanzania, Harrith Chunga Misonge (12) ndiye Mtanzania pekee anayeiwakilisha Tanzania katika michuano maarufu ya Games of the future iliyoanza jana jijini Kazan Russia.

Harrith ambaye ni mwanafunzi katika shule ya Aghakhan Mzizima jijini Dar es salaam anaiwakilisha Tanzania katika michuano ya soka huku nchi zaidi ya 120 zikitoa wanamichezo mbalimbali katika michezo mbalimbali iliyofunguliwa jana jijini Kazan.

Kinda huyo ambaye mwaka jana alitamba katika michuano ya Gothia nchini Sweden, anatazamiwa kuunda timu ya wachezaji wenzake watano watano kutoka mataifa mengine kwa ajili ya kuwania zawadi mbalimbali katika michuano hiyo mikubwa nchini Russia.

Licha ya kuwepo kwa baridi kali na kumwagika kwa barafu katika jiji la Kazan, Harrith aliyeambatana na wazazi wake amesema ana matumaini ya kufanya vyema katika michuano hiyo baada ya kupata uzoefu kwenye michuano ya Gothia iliyofanyika Julai mwaka jana nchini Sweden.

"Sina wasiwasi kwa sababu mwaka jana nilikuwa nchini Sweden na nikafanya vizuri. Hali ya hewa hainisumbui licha ya kwamba ninatoka katika nchi ya joto, mwaka jana nilizoea nilipokuwa Sweden," Alisema Harrith anayecheza nafasi ya kiungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live