Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinda Mtanzania akutana na 'live' na nyota wa Arsenal

Kinda Mtanzania Akutana Na 'live' Na Nyota Wa Arsenal Kinda Mtanzania akutana na 'live' na nyota wa Arsenal

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kinda wa Tanzania, Harrith Chunga Misonge aliyepo Russia anakoshiriki mashindano ya Games of the Future amekutana na staa wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Russia, Andre Arshavin ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mechi za mashindano hayo jijini Kazan.

Arshavin alionekana kuvutiwa kimaongezi na Harrith ambaye ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Aghakhan ya jijini Dar es salaam na kuzungumza naye kwa dakika zisizopungua kumi

“Aliniuliza nafasi ninayocheza lakini pia aliniuliza nchi ninayotoka akaniambia kwamba amewahi kufika Zanzibar na alivutiwa na fukwe zake alizozifananisha na fukwe za Maldives,” alisema Harrith.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 12 amewekwa katika timu ya Franklins Bumblebee ambayo inajumuisha wachezaji watano kutoka katika mataifa mbalimbali duniani huku akionyesha kiwango cha kuvutia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live