Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinda Man United aikataa Hispani amfuata Messi

Garnacho Decide Argentina Alejandro Garnacho Ferreyra

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipaji walichokipoteza Atletico Madrid Alejandro Garnacho Ferreyra (19), moja ya vijana wanaokuja vizuri sana katika soka la ulaya.

Mzaliwa wa hispania pale jijini Madrid na alikulia kwenye Academy ya Atletico Madrid hadi alipojiunga na Mashetani wekundu mwaka 2020 akiwa na umri wa miaka 16 tu.

Unabaki kujiuliza alifikaje Argentina ? Baba yake na Garnacho ni Muhispania halisia kabisa na Mama yake Garnacho amezaliwa bara la amerika kusini katika nchi ya Argentina, hiii ndio sababu ya yeye kuichezea Argentina alimfuata Mama alipo.

Uwezo wake na ufundi wake mguuni hasa pale anapokuwa na mpira utabaki ukisema hakika hii ni ZAWADI kwa taifa la Argentina.

Moja ya mahojiano ambayo alifanyiwa Alejandro Garnacho alisema "Scaloni aliniuliza kama nina wasiwasi,ananiambia nitulie, nicheze ninavyojua na atanipa NAFASI na huwa ninapocheza soka najaribu kuwa mimi, wachezaji wenzangu no wananisaidia ikiwa mazoezini hata kwenye mechi za kimashindano”

Ni mmoja wa vijana wenye umri mdogo na wenye kiu ya mafanikio watakaokuja kusumbua baadae

Sio kwa Manchester United tu hata kwenye Taifa lake la Argentina akiwa na vijana wenzake Alex Mac Allister, Enzo Fernandez, Julian Alvarez, Nahuel Molina, Lisandro Martinez, Federico Redondo n.k.

Kwa pesa ambayo Manchester United wametumia kumsajili Garnacho unaweza sema ni kama

Wamemchukua bure ni kiasi cha €465,000 hii ni sawa na Pesa za Kitanzania 1.2B kwa soko la usajili ulaya lilivyo kwa sasa ni pesa ndogo sana.

Siri ambayo wengi hawaijui kuhusu kijana huyu Mataifa mawili huko nyuma Hispania na Argentina yalikuwa yakimgombania kabla ya yeye

Kufanya maamuzi juu ya hatma yake ya Taifa gani atalitumika.

Garnacho ameliwakilisha taifa la Hispania chini ya miaka 18 na ameliwakilisha taifa la Argentina chini ya miaka 20, na sasa imekua rasmi Garnacho atalitumia taifa la Argentina baada kucheza kwenye kikosi cha wakubwa

kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Austalia ambapo Argentina aliondoka kifua mbela kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0.

Alejandro Garnacho Mali Ya Argentina

Chanzo: www.tanzaniaweb.live