Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinda Cambiasso apata dili England

Cambi Pic Data Kinda Cambiasso apata dili England

Fri, 24 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Kinda Omary Mvungi, kutoka kituo cha kukuza na kulea vipaji cha Cambiasso Sports  amepata dili la kwenda kucheza soka nchini England.

Mvungi anaenda nchini England katika kituo cha Garuda select project kilichopo chini ya nahodha wa zamani wa Chelsea Dennis Wise na atakua huko kwa miezi isiyopungua sita akiendelea kunolewa huku akitafutiwa timu Ulaya.

Akizungumza na Mwanaspoti dakika chache kabla ya Mvungi Kuondoka, Kaimu Mtendaji mkuu wa Cambiasso, Twaha Ngwabi ameeleza kuwa huo ni muendelezo wa kituo hicho kukuza vipaji na kuvitafutia timu.

“Tumekuwa tukifanya hivi kwa wachezaji mbalimbali na tumefanikiwa kuwapatia timu, tunafanya hivi kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa na wachezaji wengi bora na wenye uzoefu watakao isaidia timu ya taifa katika siku za usoni,” amesema Ngwabi.

Sambamba na hilo, Mvungi aliambatana na Louis Frederic Moudourou kutoka kituo cha  Rainbown cha nchini Marekani ambao wameshirikiana na Cambiasso kumtafutia fursa hiyo na kuwaahidi watanzania kuwa hatawaangusha.

“Nashukuru kwa kupata fursa hii, naenda kuonesha kile nilichonacho kwa nguvu zote, niwaahidi watanzania kuwa sitowaangusha kwani najiamini na nitafanya vizuri,” amesema Mvungi.

Kabla ya kwenda huko, Mvungi kwa nyakati tofauti amekuwa akizitumikia timu za taifa za vijana chini ya miaka 17 na 20.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz