Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinda Barcelona aliekwenda chooni akafanyiwa "Sub"

Lamine Yamal X Xavi Kinda Barcelona aliekwenda chooni akafanyiwa "Sub"

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kinda wa Barcelona Lamine Yamal alisherehekea ushindi wa kihistoria kwa upande wake dhidi ya Porto katika mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya Jumatano usiku, lakini alilamizika kutoka nje ili kwenda chooni.

Kinda huyo alicheza dakika zote katika mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo dhidi ya Porto wakiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akiwa na umri wa miaka 16 na siku 83, kinda huyo amekuwa mchezaji wa kwanza mdogo zaidi kuanza katika michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya akivunja rekodi ya Celestine Babayaro aliyoweka msimu wa 1994-1995.

Aidha, wakati Barcelona inaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kiamini na Ferran Torres kupindi cha kwanza dakika za mwisho kabla ya kwenda mapumziko kinda huyo alitumia mwanya huyo akaenda chooni.

Ilipofika dakika ya 71 ya mtanange huo kinda huyo alilazimika kutoka uwanjani kwenda chooni kwa mara nyingine wakati mechi inaendelea.

Lakini Yamal hakurejea kuendelea na mechi kwani kocha Xavi Hernandez alimfanyia mabadiliko dakika ya 80 huku Barcelona ikicheza ikiwa pungufu dakika 10 kabla ya mechi kumalizika.

Xavi alielezea kilichotokea kwa kinda huyo baada ya mechi kumalizika kwa ushindi: "Lamile Yamal alikuwa hasijisii vizuri. Alikuwa anaumwa, aliniambia jambo muda tu, alikwenda kipindi cha mapumziko, lakini mwisho wakaniambia alishindwa kabisa kurudi uwanjani kuendelea na mechi."

Barcelona ilitoboa mechi yao dhid ya Porto licha ya Gavi kulimwa kadi nyekundu dakika za lala salama na kukaa kileleni katika msimamo wa kundi lao baada ya kushinda mechi mbili mfululizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live