Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinda Azam atimkia Israel

Novatus+pic Kinda Azam atimkia Israel

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

Kiungo chipukizi wa Azam, Novatus Dismas ameondoka nchini jana Jumatano na kwenda  Israel kwaajili ya kupata mafunzo katika klabu Maccabi Tel Aviv FC inayoshiriki Ligi kuu nchini humo.

Dismas amekwenda katika timu hiyo si kufanya majaribio bali amepata mwaliko maalumu ulitumwa tangu Septemba 3, ila alishindwa kwenda kwa wakati kwa sababu ambazo hazikuelezwa.

Ofisa habari wa Azam Fc, Thabiti Zakaria ‘Zaka za Kazi’, alisema Dismas amekwenda Maccabi Haifa si kufanya majaribio bali katika mwaliko ambao atakuwepo huko mpaka Septemba 25.

Zaka alisema kama Dismas atafanya vizuri katika mwaliko huo itakuwa faida kwake pamoja na klabu kwani Uongozi wa timu hiyo unaweza kumuhitaji na kutaka kumsajili.

“Itakuwa Faida kwa klabu kama atarudi hapa nchini kutokana na mafunzo au mechi ambazo atacheza zitampa uzoefu ambao atakuja kutoa mchango katika timu,” 

“Tunaimani jambo hili ni kubwa kwake kwani mbali ya uzoefu, maandalizi ya kutosha ambayo atayapata Ulaya, mafunzo, mechi za kirafiki na mazoezi ambayo atafanya atakuwa amepata vitu vingi vya kiufundi,” alisema Zaka.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz