Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinachosababisha Guede asifunge mabao ni hiki?

Joseph Guede Yanga Kinachosababisha Guede asifunge mabao ni hiki?

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna sababu nyingi ambazo zinafanya mshambuliaji au mchezaji wa nafasi yeyote kuweza kukosa goli ndani ya uwanja hasa anapopata nafasi ya kuweza kufunga au anapokuwa kwenye eneo ambalo kwa kiasi kikubwa linahesabiwa kama anaweza kufunga.

Mfano wa sababu ambazo zinaweza kufanya mchezaji ashindwe kufunga ni pamoja na;

1.Mchezaji kukosa utulivu anapokuwa eneo la kufunga au anapopokea mpira wa kufunga.

2.Kukosekana Kwa ujasiri

Mchezaji asipofunga mara kadhaa huwa ujasiri wake mbele ya goli unapungua lakini pia Kwa mazingira haya haya wachezaji wengine kwenye 1v1 au kwenye kurupushani za kufunga huwa wanaogopa kuumia (huwa na hofu) matokeo Yake hupoteza nafasi ya kufunga.

3.Kutokufanyia mazoezi

Baadhi ya washambuliaji huwa hawafanyi mazoezi ya kufunga mara kwa mara, mpira wa kisasa unahitaji mchezaji kujitoa zaidi ndio maana baadhi ya waalimu hufanya mafunzo mengi ya kufunga kwa washambuliaji wao mfano mshambuliaji mmoja kwa walinzi 2-3.

4.Uwezo mdogo wa mchezaji kiufundi

Wachezaji wengi wenye uwezo mdogo wa kufunga wanakuwa na shida ya kuamua aweze kupiga mpira Kwa ufundi gani ili kuweza kuingia golini.

Mshambuliaji anawezaje kurudisha au kuimarisha uwezo wake wa kufunga?

1.Kufanya mazoezi ya kufunga

2.Kujiamini anapokuwa mbele ya goli

3.Kuimarisha uwezo wake wa kimbinu (technique) hasa kwenye upigaji wa mpira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live