Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinachompa jeuri Kibu Denis kusepa Simba ni hiki

Kibu Denis Carlos Kinachompa jeuri Kibu Denis kusepa Simba ni hiki

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwenye mkataba wa Kibu Denis na Simba SC kuna kipengele walichokubaliana kuwa, akipata timu Ulaya aruhusiwe kuondoka. Kipengele hicho ndicho kinampa uhakika na jeuri ya kuondoka katika klabu ya Simba.

Klabu ya Kristiansund BK imeandika barua rasmi kwenda Simba SC ili kumnunua mchezaji huyo kwa kuzingatia kipengele hicho kilichopo kwenye mkataba.

Kibu akizungumza na kituo cha Crown fm amemkataa Rashid Yazidi aliyekuwa akifanya interview na media mbalimbali akisema kuwa yeye ni msimamizi wake.

"Rashid sio meneja wangu wala sio chochote, nilimkaribisha nikampa kazi kama mwanasheria ila hakuwa mwanasheria wangu nilimwita ili afanye kazi ila tulimalizana, simdai wala hanidai, simjui. Wakala wangu ni Carlos Mastermind," amesema Kibu Denis Prosper.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live