Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinachomnyima namba Skudu kwa Gamondi ni hiki

Zdv Skudu Yanga Kinachomnyima namba Skudu kwa Gamondi ni hiki

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Skudu Makudubela anapata wakati mgumu kupenya kwenye Kikosi cha kwanza cha Miguel Angel Gamondi kwa sababu kocha huyu ni muumini wa mchezaji ambaye ana faida wakati timu yake haina mpira mguuni.

Gamondi anataka mchezaji ushiriki kusaka mpira pindi tuu ukipotea kwenye himaya yenu, jambo kubwa unalotakiwa kufanya ni kuanza kumnyima mpinzani wako nafasi ya kupitisha mpira ukiwa kwenye himaya yake .

Skudu hawezi kufanya kazi hiyo kwa sababu yeye ana enjoy zaidi kucheza Soka Mpira ukiwa katika himaya yake na ukimpotea Hana uwezo wa kuutafuta.

Nyota huyu amekosa nafasi ya kucheza Yanga Kwa sababu ya sababu za ki mfumo tuu lakini si kiwango chake kidogo, yule Maxi Nzengeli, Augustine Okrah na nyota wengine wote wanaocheza pembeni pale Yanga Wana faida hata timu yao ikipoteza umiliki wa mpira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live