Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinachomharibia Benchikha Simba ni hiki

Benchikha After Kinachomharibia Benchikha Simba ni hiki

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vyombo kadhaa vya habari vya Algeria jana vimejadili nafasi ya Kocha Abdelhack Benchikha ndani ya Simba ambaye inaelezwa uungwaji Mkono kwenye timu hiyo upo mashakani.

Inaelezwa tayari kumeanza kupata mgawanyiko kuhusu usalia ama maondoko ya kocha huyo baadhi wakiona yeye ni chanzo cha mdororo wa matokeo ndani ya timu hiyo.

Baadhi ya taarifa zinaeleza mashaka yameongezeka baada ya mkufunzi huyo kunukuliwa akisema kikosi cha Simba ni finyu na wachezaji baadhi kikosini hawana uwezo mkubwa kiasi cha kulazimika kuwatumia tu kwa sababu ndio waliopo kitendo ambacho kinaelezwa kupokelewa tofauti na baadhi ya watu wenye nguvu ya kimaamuzi ndani ya timu.

Abdelhack Benchikha ni pendekezo la klabu ya JS Kabylie na CR Belouzdad na wanafuatilia kwa karibu hali yake ndani ya Simba huku baadhi ya timu za Misri pia zikihusishwa naye.

Kituo cha Radio Dzair Chaabia cha Algeria kimetoa tetesi nyingi kuhusu Benchikha kuwa huenda akasainiwa na moja ya timu kubwa za Misri (Zamalek au Ahly) ambao nao mwenendo wao umekuwa wa mashaka kwa mashabiki wa timu hizo.

Baada ya klabu ya Ahly kupata matokeo magumu kwenye Cairo Derby na mchezo wa kabla wa Ligi mashabiki na vyombo vya habari vya Misri vilimpigia upatu kocha huyo kutwaa pahala pa Marcel Koller wa Al Ahly.

Klabu ya Simba imekuwa kwenye mdororo mkubwa wa matokeo kwa sasa baada ya kucheza mechi 5 mtawalia pasi na kupata ushindi hali inayoelezwa kuibua sintofahamu juu ya Benchikha.

Siku aliyotambulishwa niliwaambia huyu ni kocha mkubwa ambaye huwa si mstahamilivu sana mambo yakiwa hayasomeki. Ni mwepesi wa kunyanyua mabegi asipopaelewa anapopatumikia Huyu ni TOP GAFFE

Muda utazungumza ukweli punde.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live