Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinachoipa kiburi Yanga ni hiki

Yanga 6 WA0005 Kinachoipa kiburi Yanga ni hiki

Mon, 26 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukiachana na uwekezaji unaofannywa na klabu ikiwemo kusajili wachezaji wa daraja la juu lakini kuna sababu muhimu ambazo zinapelekea klabu kuwa hatari kwenye mashindano.

Technical, Kocha na benchi lake la ufundi wanapokuwa sehemu ya mechi kazi yao ni kusoma mchezo na kuona kwa namna gani mbinu zinafanya kazi, pale Yanga kwenye eneo la Technical kuna Gamondi ambaye ni kocha mkuu pamoja na Mussa Nd'aw hawa wote kazi yao kubwa ni kuhakikisha wachezaji wanatekeleza mbinu za kiufundi.

Tactical, Baada ya kuwa na wataalamu kwa maana ya Technical bench kinachofata ni uwepo wa tactical, mbinu ambazo kocha na benchi lake watazitumia kuelekea mechi tofauti tofauti (mbinu) Gamondi ameonyesha kuwa ni tajiri wa mbinu anaweza kucheza aina yeyote ya football kutokana na aina ya wachezaji aliokuwa nao na aina ya mpinzani anayecheza naye, kama ni mechi ya kuzuia atafanya hivo, kama ni Kushambualia atafanya hivo.

Physicy, wachezaji wanatakiwa kuwa na utimamu wa mwili ili kuweza kushindana dakika zote 90 kwenye uwanja, kitu ambacho Yanga sc pia wanacho, wanachezaji ambao wapo vizuri kwenye hilo eneo ndiomaana mara nyingi timu nyingi zinapokutana na Yanga sc zinashindwa kuhimili kasi ya mechi wakati huo Yanga wakitumia kama faida ya kupata ushindi.

Mentality, Hiki ndo kitu muhimu zaidi kwenye mpira utimamu wa akili ndo unaamua mchezaji anacheza vipi kwenye mechi, Yanga wanaonekana kufaulu kwenye hilo eneo wachezaji wote wa kikosi cha Yanga wana ile winning mentally kuwa hii klabu inatakiwa kushinda karibia kila mechi hivo wanaopata nafasi ya kuanza wanatakiwa kujitoa kwa asilimia mia.

Bila Shaka Yanga Sc ndiyo timu bora kwa sasa Tanzania, na ni miongoni mwa Timu bora barani Afrika, Takwimu zinatwambia katikati misimu mitatu iliyopita, wametwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania mara (3), Kombe la ASFC na CRDB mara (3), ngao ya hisani mara (2). wakati katikati michuano ya kimataifa kwa mara ya kwanza wamefanikiwa kucheza fainali ya Kombe la shirikisho Afrika huku wakicheza robo fainali ya Klabu bingwa barani Afrika baada ya zaidi miaka (20).

Nyuma ya mafanikio na mwendelezo mzuri wa Yanga SC kuna vitu muhimu vinne. Uongozi imara, chini ya Engineer Hersi Said. uwekezaji imara, chini ya Ghalib Said Mohamed (GSM). Benchi imara la ufundishi chini ya Kocha mkuu Miguel Gamond kwa sasa, na kikosi imara kinachoundwa na mastaa wengi kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika.

Utelelekezaji mzuri wa majukumu kwenye kila idara imekuwa chachu kubwa ya mafanikio, GSM anatoa pesa, Hersi Said anasimamia malengo na mwelekeo wa timu (vision na mission), wakati benchi la ufundi na wachezaji wakitekeleza jukumu lao mama uwanjani kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri na mafanikio.

Ukiangalia kikosi cha Yanga msimu huu unaiona taswira halisi ya kile walichokifanya misimu Takribani mitatu iliyopita, ukiangalia zaidi uimara wa kikosi chao hasa namna walivyofanya maboresho unaiona nafasi ya wao kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya kimataifa. Kitu pekee Yanga wanatakiwa kuzingatia ni mwendelezo mzuri wa hiki wanachokifanya.

Naiona nafasi kubwa ya Yanga kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa msimu huu lakini naiona nafasi kubwa ya kufanya vizuri zaidi kwa misimu ijayo. (Perseverance, Patience and Consistency) ni njia muhimu kwao kufika nchi ya Ahadi. Mpira ni mchakato (Football is process...)

Zaidi nafikiri huu ni muda sahihi sana kwa mashabiki kuwa karibu na kuipa nguvu timu yao. Bidhaa za GSM, Kadi ya uwanachama, Kuingia viwanjani ndiyo mafanikio yenyewe klabu.

Ukweli ni Kwamba hiki wanachokifanya yanga kwa sasa ni darasa huru, ni maamuzi ya kila mtu kushika kalamu. Kichwa cha habari kinasomeka. Uwekezaji imara, uongozi imara, benchi la ufundi imara na kikosi imara ndiyo njia ya mafanikio.

Yanga wanazidi kuwa bora kwasababu wameimarisha misingi muhimu inayopelekea timu kupata ushindi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live