Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinachoendelea kwa Mpole DR Congo

Mpole George Bb Kinachoendelea kwa Mpole DR Congo

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa FC Lupopo, Mtanzania George Mpole amesema Ligi Kuu ya DR Congo imefikia hatua ya mtoano ilkusaka bingwa wa nchi.

Ligi ya nchi hiyo inachezwa kwa kanda mbili ile ya Lumbumbashi inawakilishwa na TP Mazembe, FC Lupopo, Lubumbashi Sport na Don Bosco ilhali ukanda wa Kinshasa ni AS Vita, Maniema, AF Congo na Douphine Noir, jambo ambalo Mpole amesema ligi ilipofikia ni ngumu ikiwa inahitaji hesabu kali ili kupigania ubingwa wa nchi.

"Kwenye mechi nne tulizocheza tumetoka suluhu mbili na tumeshinda michezo miwili. Katika hizo nimefunga mabao matatu na nimetoa asisti moja kabla ya kufika kwenye hatua ya mtoano, nilifunga mabao matatu kwenye michezo tisa," amesema.

"Ili kuthibitisha hatua ya mtoano ni ngumu kupata bingwa wa nchi, ligi imeanza kuonyeshwa tofauti na mwanzo ambapo ilikuwa haionyeshwi, kila timu inahitaji nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya CAF."

Kwa Mtazamo wa Mpole timu anazoziona zina nafasi kubwa za kunyakua taji hilo ni timu anayoichezea na TP Mazembe.

"Japokuwa mpira ni dakika 90, hizo timu mbili zina ushindani mkali sana," amesema.

Msimu wa 2021/22 Mpole kabla ya kujiunga na FC Lupopo akiwa na Geita Gold aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa mabao 17, akimuacha bao moja nyuma aliyekuwa straika wa Yanga, Fiston Mayele aliyemaliza na 16.

Kiwango alichoonyesha kilizishawishi Simba na Yanga kuhitaji huduma yake na aliwahi kuzungumzia hilo akisema, "ni kweli nilifanya mazungumzo na Simba ila mambo hakwenda sawa".

Pia 2022 aliitwa kwenye kikosi cha timu ta Taifa 'Taifa Stars' kilichocheza Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).

Chanzo: Mwanaspoti