Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kimyaa wametulia

Yanga Final Results Fiston Mayele akiwataabisha walinzi wa Mbeya Kwanza

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndivyo unavyoweza kusema baada ya vinara wa Ligi Kuu Bara 2021/2022, timu ya Yanga kutoka kifua mbele ugenini Mbele ya wageni wa Ligi timu ya Mbeya Kwanza.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Kumbu kumbu ya Sokoine Jijini Mbeya, ulishuhudia ukimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 2-0.

Magoli yote ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa kipindi cha Kwanza, la kwanza likiwekwa kambani na Saido Ntibazonkiza 18' kwa mpira wa adhabu na la pili likiwekwa kambani 30' na Straika katili wa nyavu Fiston Mayele.

Mchezo huo ulikuwa ni mzunguko wa saba wa Ligi kuu na katika michezo yake saba yanga imeshinda michezo sita na kutoa sare mchezo mmoja dhidi ya Namungo kule Ilulu Mkoani Lindi.

Kwa ushindi huo wa leo Yanga inazidi kujikita kileleni kwa alama zake 19 baada ya kucheza michezo saba.

Mbeya Kwanza wanabaki katika nafasi yao ya 11 wakiwa na alama saba wakiwa wameshacheza michezo 7.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live