Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kimmich ajutia kukataa Chanjo ya Covid- 19

Kimmich Joshua Kimmich

Mon, 13 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Bayern Munich Joshua Kimmich amekiri kwamba anajutia kwa kupuuzia kuhusu kupata chanjo ya COVID-19.

Kimmich ambaye mwezi Oktoba alijitokeza na kudai kwamba hawezi kupata chanjo dhidi ya Corona Virus ambaye baadaye alilazimika kukosa michezo mingi ya Bayern baada ya kuonekana ameingiliana na mtu ambaye alikutwa na maambukizi.

“Inawezekana nitachukua chanjo siku zijazo,” Kimmich alisema mnamo Oktoba, akielezea kuwa badala yake alikuwa akichukua vipimo vya PCR kila siku nyingine na kufuata taratibu kali.

Mwishoni mwa Novemba, Kimmich mwenyewe alipimwa na kukutwa na maambukizi. Ambapo hajaichezea timu yake hadi 2022 kwa sababu ya athari za virusi kwenye pafu lake, ingawa ameanza tena mazoezi mepesi.

Alisema alipoteza hisia zake za kuonja na kunusa alipokuwa mgonjwa na hatacheza hadi mwezi ujao kwa sababu ya maji kwenye mapafu kufuatia maambukizi.

Kimmich aliiambia ZDF: “Kwa ujumla, ilikuwa vigumu kwangu kukabiliana na hofu na wasiwasi wangu, na ndiyo maana nilibaki bila kuamua kwa muda mrefu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live