Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kimenya: Sitowaangusha Stars

78568 Pic+kimenya

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIRAKA Salum Kimenya anayeichezea Tanzania Prisons, amerejeshwa katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars  kilichopo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije na nyota huyo amesisitiza hatawaangusha akiwa ndani ya timu hiyo.

Kimenya amerejeshwa katika kikosi ambacho kimeitwa kwaajili ya mchezo wa kirafiki Oktoba 14 dhidi ya Rwanda,  pia kikijiandaa na mchezo wa CHAN dhidi ya Sudan.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kimenya alisema ana furaha kuona ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa, kwani ni jambo ambalo siku zote anatamani kuliona katika maisha yake ya soka.

"Ni suala zuri mno na namshukuru Mungu kwasababu yeye ndio kila kitu, lakini pia Mwalimu Ndayiragije  kwa kumuona na kuamini ataendana na falsafa yake," alisema.

Kimenya aliongeza kwa kwa heshima aliyopewa na kocha huyo ya kumrejesha katika kikosi cha timu ya Taifa,ameahidi kuonyesha heshima kwa vitendo akiwa katika jezi ya timu ya Taifa.

Kimenya mara ya mwisho kuitwa katika timu ya Taifa ni katika kikosi kilichocheza na Lesotho kikiwa chini ya kocha Emmanuel Amunike aliyefurushwa mara baada ya timu hiyo kurejea kwenye Fainali za Afcon 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz