Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kimataifa bado hatujui tunataka nini

Chama Vs Vipers Clatous Chama akiwa katika majukumu yake Uwanjani

Fri, 10 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maneno ni mengi kuhusu kiwango cha Simba kwenye mchezo wa jumamosi dhidi ya Vipers kwa Mkapa, Wengi wanabeza kiwango kile. Muhimu kwa Simba ni alama tatu ambazo zimeweka hai matumaini ya kufuzu hatua inayofuata.

Bahati mbaya sana sasa hivi kuna mstari mwembamba sana kati ya mchambuzi na shabiki kwa kuwa wachambuzi nao wanapita mulemule. Nitakuambia kitu.

Simba kaupiga mwingi pale Guinea kisha akaishia kupasuka... unakumbuka wanaoponda sasa walisema nini? (Tunataka matokeo sio kuupiga mwingi) Simba kaja kupasuka nyingi hapa dhidi ya Raja Casablanca wakasema nini..? (Timu ina wazee wengi)

Simba kaenda kushinda St Mary's Stadium-Kitende wakasemaje..? (Simba kashinda ila kacheza mpira mbovu)

Jana kashinda tena bado kelele ni kiwango kibovu...Sasa mnataka kiwango bora au matokeo?Unataka biriani au alama 3?

Okay.Tunataka Simba aendelee kuupiga mwingi kama alivyoupiga dhidi ya Horoya na afungwe au acheze kimkakati ashinde asonge mbele? [Majibu wanayo wao].

Mimi nadhani,Tunaposema Vipers wabovu tusisahau huyu Vipers hakufungwa dhidi ya Tp Mazembe mechi mbili (Ugenini na nyumbani) na ndiye aliemtoa CAFCL. Tusisahau huyu Vipers hakupigiwa kura kufika hapo alipo alipambana.

Wanaojua mpira wanajua huwezi kuwa bora kila siku na kila mchezo ndio maana Argentina alifungwa na Saudi Arabia na bado akawa Bingwa wa Dunia...hapo hapo England na Hispania walitembeza kichapo baadhi ya mechi, na walipoishia kila mtu anajua.

Horoya alitoa game nzuri sana dhidi Raja AC kule Morocco, kirahisi sana ungedhani wangeshinda au kutoa sare nyumbani kwao...lakini wamepasuka 3.

Nafikiri tuwapongeze kwanza Simba kwa kushinda kisha performance ije baadae japo mkakati kwenye haya mashindano ni kushinda kwako kwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live