Mwanamitindo na mfanyabiashara Kim Kardashian, ameeleza kuwa aliyekuwa mume wake Kanye West kwa sasa amebadilisha mtindo wake wa kuishi.
Kim ameyasema hayo kupitia kipindi chao kipya cha TheKardashians wakati yeye na dada yake #Kourtney wakiongea kuhusiana na maswala ya malezi ya watoto, #Kim amedai kuwa mume wa zamani Kanye West kwa sasa amebadilika na amechagua kufanya anasa kidogo na kuzidisha muda wa kukaa na binti yao North West.
Huku mwanamitindo huyo akidai kuwa kwa sasa binti yake anafurahia sana kupata muda mwingi wa kukaa na baba yake.
#KimKardashian, ameendelea kuupiga mwingi katika #bland yake ya #SKIMS baada ya kuingia mkataba wa kutengeneza nguo za ndani na #NBA.