Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kim aweka rekodi mpya Taifa Stars

Taifa Stars Safari Taifa Stars

Mon, 11 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ushindi wa bao 1-0 ambao Taifa Stars imepata ugenini dhidi ya Benin jana umemfanya kocha Kim Poulsen kuvunja rekodi ya mafanikio aliyoyapata kwa timu hiyo wakati ilipokuwa katika harakati za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.

Rekodi hiyo ni ile ya kukusanya idadi kubwa ya pointi katika hatua ya makundi ambayo ni ya pili kwenye mashindano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia kabla ya ile ya mwisho ambayo inatoa timu tano (5) za kuiwakilisha Afrika katika fainali hizo ambazo zina thamani na hadhi kubwa zaidi katika ngazi ya timu za taifa duniani.

Matokeo hayo ya jana dhidi ya Benin, yameifanya Taifa Stars ifikishe pointi saba na kuongoza msimamo wa kundi J baada ya kuibuka pia na ushindi dhidi ya Madagascar nyumbani na kupata sare moja ugenini dhidi ya DR Congo.

Wakati inawania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 ikiwa chini ya Kim Poulsen, Taifa Stars ilimaliza ikiwa imekusanya jumla ya pointi sita (6) na kushika nafasi ya tatu kwenye kundi C lililokuwa na timu za Morocco, Ivory Coast na Gambia.

Stars ilianza kwa kupoteza kwa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Ivory Coast, ikaja kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 nyumbani ilipocheza na Gambia na mechi ya tatu ikapata ushindi wa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Morocco

Pointi hizo sita ilizokusanya katika mechi tatu za mwanzo ndizo ambazo Stars ilimaliza nazo kwani ilipoteza mechi zote tatu za mwisho ambazo ni mbili ugenini dhidi ya Gambia na Morocco na moja ya nyumbani dhidi ya Ivory Coast.

Ilifungwa mabao 2-1 na Morocco, ikapoteza kwa mabao 4-2 nyumbani na Ivory Coastal na mechi ya mwisho ikafungwa mabao 2-0 ugenini na Gambia.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz