Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kim ajipanga mapema

Yondan Kimpic Data Kim ajipanga mapema

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA wa timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars', Kim Poulsen amesema katika siku mbili za mazoezi yake amekuwa akiwafundisha wachezaji namna ya kujilinda na kushambulia.

Stars ilianza mazoezi jana Jumanne Machi 9,2021 asubuhi wakifanya mazoezi asubuhi na jioni uwanja wa Benjamini Mkapa.

Kim amesema ameonesha kufurahishwa na kiwango cha wachezaji wake mazoezini akiamini watapambana na kuivusha timu kwenye Fainali za Afcon.

“Wachezaji wapo vizuri na nimekuwa nikiwafundisha namna ya kujilinda pamoja na kushambulia, zoezi limeonekana kwenda vizuri”.

“Nimechanganya wachezaji wazoefu na vijana kitu ambacho nimekiona kikienda vizuri katika pande zote mbili”.

Kocha huyo alimalizia kwa kusema kuwa; “Wachezaji ambao hawajafanya mazoezi leo ni wawili tu, ambao wote wana majeraha,".

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz