Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kim Poulsen atangaza Kikosi cha Stars

Poulsen Kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi Cha wachezaji 27 kwa ajili ya michezo miwili ya mwisho ya kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia Qatar 2022.

Taifa Stars itashuka dimbani Novemba 11 dhidi ya DR Congo na baadaye kucheza na Madagascar Novemba 14, 2021.

Kinara kutoka katika kila kundi ndie atakaefuzu kwa hatua itakayofuata, ambapo zitapatikana timu 10, zitakazocheza michezo miwili nyumbani na ugenini ambapo zitapatikana timu tano zitakazokwenda Kombe la Duni kwa Bara la Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live