Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kiluvya FC hawajaridhika na kipigo cha bao 6-0 kutoka kwa Yanga

Yanga X640.png Kiluvya FC hawajaridhika na kipigo cha bao 6-0 kutoka kwa Yanga

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Kiluvya, Mussa Nota amesema wanaomba kukutana na Klabu ya Yanga kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam msimu huu ili walipe kisasi.

Nota amesema hayo mara baada ya timu yake kupokea kipigo cha bao 6-0 kutoka kwa Yanga Sc, jana Jumamosi ikiwa ni mchezo wa kirafiki wa kujiweka sawa kwa Yanga kabla ya kuwavaa Al Merrikh ya Sudan kwenye mchezo wa CAFCL utakaopigwa Septemba 16, 2023 nchini Rwanda.

Ofisa Habari wa Kiluvya FC akiwa katika studio za Wasafi FM, jana usiku amesema; "Kiukweli tumepigwa dozi (6-0) nisiwe muongo tulizidiwa ila tumecheza vizuri. Kama timu za ligi kuu zilipigwa tano tano sisi kufungwa (6-0) na wababe wa ligi kuu (Yanga) ni jambo kubwa la kujivunia.

"First League inakaribia kuanza sisi kama Kiluvya FC tumefurahi kupata mechi hii dhidi ya Yanga. Nikuahidi tu (Mkai) kisasi tutalipa kuanzia first league hadi (FA). Naomba Mungu tukutane na Yanga (FA) tulipe kisasi. Naamini tutakutana tu (FA)," amesema Mussa Nota.

Swali: "Kisasi? Huogopi pira Gamondi, watu wanapigwa tano tano, kumi nawewe umepigwa sita. Huogopi?," amehoji Paul Mkai mtangazaji wa Wasafi Media.

Jibu: "Mkai, wametuzidi ubora hata maneno watuzidi kweli? Nilimwambia rafiki yangu Ali Kamwe msituwekee kikosi (B) tunataka mastaa wacheze ili tukifungwa tujue panapo vuja nashukuru walifanya hivyo. Kiluvya FC ni timu ya jeshi iko First league tunakuja kwa kishindo huko juu," amesema Mussa Nota.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: