Kilimanjaro. Mzuka wa mbio za Kilimanjaro marathoni umesababisha mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro kufurika wageni huku baadhi ya huduma ikiwamo nyumba za wageni kuadimika.
Baadhi ya watu waliojitokeza kushiriki mbio hizo walilazimika kwenda kulala mjini Arusha huku bei ya chini ya vyumba vya kulala ikifika Sh 40,000 mpaka 80,000 licha ya wenyeji kueleza kwamba vyumba hivyo kwa siku za kawaida ni Sh 7000 mpaka 25000.
Licha ya bei hiyo, bado nyumba hizo zilikuwa adimu, achilia mbali bei ya chakula na usafiri ambayo ni mara mbili ya bei ya kawaida.
"Moshi imefurika, haijawahi kuwa hivi, sababu ya marathoni na pia kuna mkutano wa Mwakasege," alisema mmoja wa dereva bodaboda, Japhet Andrea.
Mama lishe, Anna John alisema kipindi hiki ni cha neema kwani wana uhakika wa kupata faida mara mbili.
Licha ya changamoto hiyo ya bei, washiriki wa mbio hizo wameonyesha hamasa huku wengi wao wakifurika uwanjani Alfajiri.
Pia Soma
- Wanariadha Panga, Magdalena waing'arisha Tanzania Kilimanjaro marathoni
- Mwanariadha Samson Ramadhan awachambua, Failuna, Sarah, Magdalena
- Mangula alazwa ICU, Magufuli amjulia hali