Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilimanjaro Stars, Zanzibar Heroes kukata utepe

IMG 20231212 WA0567 Kilimanjaro Stars, Zanzibar Heroes kukata utepe

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania Bara “Kilimanjaro Stars’ inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ Desemba 27, mwaka huu katika Uwanja wa Amaan Kisiwani Unguja-Zanzibar.

Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja huo ambao umefanyiwa ukarabati mkubwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Meneja wa timu za Taifa, Daniel Msangi amesema mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya kufungua Uwanja wa Amaan baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa.

“Wachezaji wa Bara watacheza kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars na wachezaji wa Zanzibar watakuwa kwenye kikosi cha Zanzibar Heroes na maandalizi yanaendelea vizuri,” amesema Msangi.

Mgeni rasmi kwenye mchezo huo anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi.

Uwanja wa Amaan umefanyiwa marekebisho makubwa na kampuni ya Orkun kwa miezi sita tu, na sasa una uwezo wa kuingiza washabiki takribani 15,000.

Chanzo: Dar24